Jeremiah 7:4-8

4 aMsitumainie maneno ya udanganyifu na kusema, “Hili ni Hekalu la Bwana, Hekalu la Bwana, Hekalu la Bwana!” 5 bKama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake, 6 ckama msipomwonea mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama msipofuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe, 7 dndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele. 8Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana.

Copyright information for SwhKC